Wednesday, June 27, 2012

RICK ROSS AONGELEA KUHUSU KUONGEZA WASANII NDANI YA MMG

                          Rick Ross akiwa na MMG members ndani ya  New York’s Hot 97 radio.

Rapa anaekimbiza pande za USA na world wide, Rick Ross ambaye pia ni kiongozi wa kundi la Maybach Music Group (MMG) amesema kwa sasa hana mpango wa kuasaini mwanamuziki yoyote bali ame concetrate katika project za members wa kundi lake. Hata hivyo amesema kadri muda unavyokwenda atazidi kusaini wasanii wakali kwani ndo mipango yake kusaini wasanii wakali ambao ni chipukizi. Rick ross aliongea hayo alipokua akihojiwa na kituo cha radio cha New York’s Hot 97pande za USA.

50 CENT ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI AFTER BAD CAR CRASH

                                            Gari aliyopatia ajali 50 cent
                   

                                               50 Cent akipelekwa hospitali

Rapa 50 cent ameruhusiwa kutoka hospital baada ya kupata ajali mbaya ya gari asubuhi ya jumanne (26.6). 50 cent alipata ajali hiyo katika jiji La NEW YORK na alipelekwa katika hospitali ya New York Hospital Queens, ambako alipatiwa matibabu haswa katika maeneo ya shingoni alipokua amepata majeraha kadhaa.