Sunday, March 2, 2014

Blog imerudi tena kazini

Baada ya kutofanya kazi kwa takribani mwaka mmoja kutokana na vikwazo mbalimbali, napenda kuwataarifu kuwa blog hii imerud tena kazini kama kawaida.

Wednesday, June 27, 2012

RICK ROSS AONGELEA KUHUSU KUONGEZA WASANII NDANI YA MMG

                          Rick Ross akiwa na MMG members ndani ya  New York’s Hot 97 radio.

Rapa anaekimbiza pande za USA na world wide, Rick Ross ambaye pia ni kiongozi wa kundi la Maybach Music Group (MMG) amesema kwa sasa hana mpango wa kuasaini mwanamuziki yoyote bali ame concetrate katika project za members wa kundi lake. Hata hivyo amesema kadri muda unavyokwenda atazidi kusaini wasanii wakali kwani ndo mipango yake kusaini wasanii wakali ambao ni chipukizi. Rick ross aliongea hayo alipokua akihojiwa na kituo cha radio cha New York’s Hot 97pande za USA.

50 CENT ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI AFTER BAD CAR CRASH

                                            Gari aliyopatia ajali 50 cent
                   

                                               50 Cent akipelekwa hospitali

Rapa 50 cent ameruhusiwa kutoka hospital baada ya kupata ajali mbaya ya gari asubuhi ya jumanne (26.6). 50 cent alipata ajali hiyo katika jiji La NEW YORK na alipelekwa katika hospitali ya New York Hospital Queens, ambako alipatiwa matibabu haswa katika maeneo ya shingoni alipokua amepata majeraha kadhaa.

Tuesday, February 28, 2012

COMMON AMALIZA BEEF NA DRAKE

         Common akiwasili kwenye tuzo za Grammy awards


Rapper Common ambaye alimdiss Drake wazi wazi kwenye nyimbo ya Rick ross (stay schemin rmx) amedai kua beef lake na Drake limekwisha. Common aliyaongea hayo kwenye red carpet ya Grammy awards na hakutoa sababu zozote za kumaliza beef hilo. Common pia aliwahi kumchana Drake katika track inayoitwa sweet.

JIM JONES MATATANI BAADA YA KUVUNJA SHERIA ZA BARABARANI





                                                Jim Jones akiwa na Juelz Santana
                                   
Jim Jones amekamatwa jumatatu (tar. 27 feb.) baada ya kugundulika kuwa antumia leseni ambayo imekwisha tumika. Rapa huko alikula pingu kwa dakika kadhaa kabla ya kuachiwa baada ya muda mchache. Msemaje wa rapa huyo alisema Jones alikamatwa kimakosa kwani yeye alikua haendeshi gari na alikua ametulia kwenye siti ya pembeni. Pia kuhusu leseni ya Jones kuwa suspended alisema anadhani kuna errors kwenye system ya leseni.